Mwakilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC, Hamid Reza Dehqaniamezitaka nchi za Kiislamu kukabiliana na makundi ya kitakfiri kama Boko Haram la nchini Nigeria.

Hamid ameongeza kuwa nchi za Kiislamu na OIC zinapasa kujiweka mbali na makundi yanayojinasibisha na Uislamu lakini badala yake yamekuwa yakitekeleza mashambulio ya kigaidi dhidi ya watu wasio na hatia.

Hamid amesema wengi kati ya wanachama wa kundi la Boko Haram si Waislamu, bali wamo Wakristo na wengine wapagani, ingawa Waislamu ni wachache kwenye kundi hilo.

Ripoti zisizo rasmi zinaonyesha kuwa, asilimia 90 ya wanachama wa kundi la Boko Haram si Waislamu.

Kundi la Boko Haram lilianzishwa mwaka 2002 na raia wa Nigeria aitwaye Muhammad Yussuf aliyesoma nchini Saudi Arabia.

Mwezi uliopita, kundi hilo liliwateka nyara wanafunzi wasichana wanaokaribia 300 katika jimbo la Borno, na hadi sasa bado halijawaachilia huru.

Neno Boko Haram lina maana ya kwamba 'Elimu ya Kimagharibi ni haramu', na lengo kuu la kundi hilo ni kuiangusha serikali ya Nigeria.

Kundi hilo limetekeleza mashambulio kadhaa ikiwemo kwenye misikiti, mashule, mahospitali, ofisi na majengo ya serikali hususan katika eneo la Kaskazini mwa Nigeria.
Radio tehran.

Post a Comment

 
Top