Uso wake Rolf Bushholz ulivyo na maumbile kama pembe.
Mwanaume mmoja kutoka Ujerumani
anayeshikilia rekodi ya dunia ya kuwa mtu aliyetoboa zaidi mwili wake,
Rolf Buchholz amekatazwa kuingia Dubai.
Rolf Bushholz aliyenyimwa ruhusa ya kuingia Dubai.
Bwana Buchholz alieleza BBC kuwa maafisa wakuu katika uwanja wa ndege walihofia huenda alikuwa ni '' mchawi'' .
Mtaalamu huyu wa tarakilishi alitambulika na kitabu cha rekodi za dunia cha Guiness, kama mwanaume aliyetoboa mwili wake zaidi duniani mwaka wa 2012.
Rolf Bushholz katika moja ya maonyesho yake.
Onyesho lake katika mgahawa maarufu wa Irque le Soir ulioko katika hoteli ya Fairmont Hotel Dubai lilifutiliwa mbali.
Mdomo wake uso wake Rolf Bushholz ulivyotogwa.
Bwana Rolf amesema kuwa mizigo yake bado iko Dubai na aliapa kwenye mtandao wa kijamii kuwa hatarudi tena katika milki za Kiarabu.
Polisi na Maafisa wa usafiri wa ndege nchini Dubai hawajazungumzia swala hilo.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.