Ghafla eneo hili liligeuka kuwa kama sehemu ambayo wakaaji walihama muda mrefu.
                                     Roli hilo baada ya ajali.
WATU watatu wamepoteza maisha na wengine watatu kujeruhiwa vibaya katika ajali iliyotokea usiku wa tarehe 16 July 2014 majira ya saa 4.00 katika kijiji cha Ugwachanya kilichopo nje kidogo ya manispaa ya Iringa, barabara ya Iringa Mbeya.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi amesema lori  aina ya Scania lenye namba za  usajili T 801 ACD lililokuwa  likielekea mkoani Mbeya liliacha njia na kugonga  kilabu cha pombe za kienyeji na kusabisha madhara hayo.
Waliofariki wametajwa kuwa ni Leonard Mkendela (35), Neema Mkendela na Kamsia Mkendela wote wa familia moja na Ester  Mwalomo na Oscar Zosama, wote wakazi wa kijiji hicho kilichopo jirani na kijiji cha Isimila yolipo makubusho ya zana za mawe.

Waliojeruhiwa ni pamoja na dereva wa roli hilo, Kasim Ahamed Mambo na tingo wake, Mussa Abdalla Kadege wote wakazi wa Kijiweni mjini Iringa.

Mwingine aliyejeruhiwa katika ajali hiyo ni Juma Abdalah Omary  anayadaiwa ndiye aliyekuwa akiendesha roli hilo wakati ajali hiyo ikitokea. ajali hiyo

Majeruhi  wote  watatu  wamelazwa  katika  Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa wakiendelea na matibabu.

Post a Comment

 
Top