Huku harakati za kutaka matumizi ya Bangi
kuhalalishwa zikishika kasi katika sehemu mbali mbali duniani, Tanzania
haijaachwa nyuma.
Mwenyeketi wa Halmashauri ya wilaya ya Makete Daniel Okoka amesema matumizi ya Bangi katika wilaya hiyo hayajaanza leo, tangu zamani watu kitamaduni walikuwa wakitumia Mbegu za Bangi kukaanga na chakula.
Na kama mmea huo ungekuwa na tahri kubwa kiafya, basi watu wengi wilayani humo wangekuwa vichaa.
Miti ya mimea hiyo pia ilikuwa ikitumiwa kutengeza kamba ambazo anasema zilikuwa za nguvu sana.
Lakini kwa sababu ya sheria kali, matumizi ya Bangi au Marijuana yanafanywa kichinichini katika wilaya hiyo.
Mwandishi wa BBC Leonard Mubali, anaandaa taarifa hiyo huko wilayani Makete na baadaye utaweza kuisikiliza katika redio na hapa kwenye mtandao.
Lakini kwa sasa tunaulijza je ni ni sawa kwa Bangi kuhalalishwa kama chakula nchini Tanzania? toa maoni yako kwenye ukurasa wetu wa Facebook:
Post a Comment