Mwandishi wa habari na mtangazaji maarufu wa kipindi cha taarabu (Mipasho) katika kituo cha redio Ebony fm Faustina Erasto  “Tinna Tana” kama anavyojiita mwenyewe, anatumia fursa hii katika kipindi cha kuelekea kufanyika kwa tamasha la Mtikisiko mikoa ya nyanda za juu kusini kwa kufikisha salaamu zake kwa mashabiki na wasikilizaji wake.

Tinna Tana amejizolea umaarufu katika medani ya uandishi na utangazaji wa redio kutokana na umahiri wake kwa kuitendea haki sauti yake na kuwaburudisha mashabiki akiwa kwenye kipindi, kitendo ambacho kimemfanya kuwa midomoni mwa maelfu ya wasikilizaji.

Tina ambaye ni mtangazaji wa kipindi cha Raha zote ambacho hurushwa na Ebony fm kila siku ya juma Mosi kuanzia saa 08:00-10-00 mchna na segment inayokwenda kwa jina Kaogeee! Katika kipindi cha Jambo Beat kuanzia jumatatu mpaka Alhamisi ambaye pamoja na kuwa kinda katika fani hiyo lakini ameteka idadi kubwa ya mashabiki.

Akizungumza mara baada ya kutembelewa mtandao huu nyumbani kwake pande za Kihesa, Tina amesema ameamua kufikisha salaamu zake kwa mashabiki wake kutokana na ushirikiano ambao wamekuwa wakimpa akiwa kazini ambapo pamoja na hayo amezungumzia ugumu wa kazi yake na kukiri kuwa mara nyingine kazi humuwea ngumu.

“Ni kweli mara nyingine huwa najikuta katika wakati mgumu katokana na staili ya vipindi vyangu si unajua tena mambo ya taarabu umbea na nini, sasa linapo kuja suala la kurekebishana tabia ndipo watu hujishuku na kufikiri nawasema wao na hasa jambo likimgusa utakuta unarudi nyumbani unakuta mtu kakununia tu.”
 


Lakini Tina pamoja na yote anawataka wanajamii kuacha kuwachukulia watangazaji kama ni watu wa kujiona bali wanachotakiwa ni kutoa tu ushirikiano hiyo ni kazi tuu! “Watu wamekuwa wakituchukulia tofauti na kudhani eti sisi tunajishaua laki wala sisi ni watu kama wao hivyo basi nawataka wananchi kutufikishia matukio ambayo yanaweza kuwa mafunzo kwa jamii”.

Umaarufu mwana dada huyu unazidi kukua siku hadi siku kutokana na bidii zake pamoja na jinsi anavyo weza kukitumia vyema kipaji alichonacho.
 Tina akiwa saloon mambo ya mapoudaaa!

"Vipindi vyangu vina maadhi ya Pwani jambo linalowafanya wakazi wa mikoa nyanda za juu kusini kuhisi kama wanaiona bahari hivi kumbe ni ukame tu hahahaa"!
Akiwa kazini..Kaogeeeeeeeee!

Post a Comment

 
Top