Vijana wengi nchini Tanzania wamejikita katika sanaa ya muziki wa kizazi kipya kama sehemu ya ajira na kujitahidi kwa kiasi fulani kuufikisha muziki huo hadi nje ya mipaka.

Lakini pamoja na kuwepo kwa aina lukuki za muziki unaoimbwa na wasanii nchini, muziki wa Hip hop ni muziki ambao unatajwa kuwa na staili yake ya pekee ya kuwasilisha na kuibua changamoto ndani ya jamii sambamba na uhalisia wa maisha na ndio maana utawasikia wanatasnia hiyo waki sema "Hip hop is a life".

Muziki huu umepata mabalozi kutoka katika kila pembe ya nchi japo idadi kubwa ya wasanii wanatajwa kutokea katika mikoa ya Kaskazini.

Lakini kutokana na ukweli kwamba wapo wasanii wenye majina makubwa kutokana na kudumu kwenye tasnia kwa muda mrefu, wapo wasanii chipukizi (Undergrounds) ambao wanafanya vizuri katika game hii lakini hawajawahi kusikika na kutamba kutokana changamoto ndani ya tasnia.

Msanii Kutoka nyanda za juu kusini Nickson joseph sanga (Dj, Nas) ambaye kwa sasa anafanya kazi katika kituo cha redio kinachofanya vizuri kutoka katika mikoa ya nyanda za juu kusini Ebony Fm kama Dj ni mwanamuziki chipukizi wa miondoko ya Hip hop ambaye kazi zake kwa sasa zimezagaa nchi nzima.

Dj, Nas ambaye kwa sasa anatamba na ngoma yake mpya aliyoipa jina la Salaam kwa Jakaya aliyoifanya katika studio za Ebony fm chini ya produser Emmo Da'pro, ambayo kwa mujibu wa maelezo yake amedai kuwa ni wimbo ambao umemfanya ajulikane zaidi ya awali na kujikuta akipigiwa kufanyiwa mahojiano na media nyingi nchini.

"Wimbo wangu umekuwa gumzo mtaani na kuzungumziwa na mashabiki kibao na kama haitoshi nimekuwa nikipigiwa nikipata usumbufu wa simu kutoka kwa mashabiki kutaka kufahamu niliwaza nini mpaka kuandika wimbo huo". katika mahojiano maalumu na mtandao huu dj Nas pia anadai kuwa yupo kwenye gemu tangu zamani lakini linapo kuja suala la kutoka bado ni kizungumkuti kwake.

Aidha mwanamuziki huyo anakiri kuwa urasimu katika media ni moja ya kikwazo kwa wasanii wadogo kusikika kazi zao. "suala zima ni mpunga (pesa), watangazaji na ma Dj wamekuwa wakizungua sana na wamekuwa wakiibania air time ngoma kama msanii haujatoa chochote.

Mbali na ngoma ya Salaamu kwa Jakaya Dj, Nas amewahi kutamba na nyimbo kama Chap chap, Kausha, Ama nini na Wanaisaliti Hip hop kazi alizozifanya katika studio tofauti kama Bantu music, Nab records na AB records.

Pamoja na changamoto hizo zinazokwamisha malengo ya kazi za wasanii chipukizi Dj, Nas ameongeza kuwa bila msanii kuwa na Manager ni vigumu sana kufanikiwa katika kazi zake.

Post a Comment

 
Top