Nani aliyefanya mauaji Mpeketo?
 Rais Uhuru Kenyatta amesema yalichochewa kisiasa lakini Al Shabaab wamekiri ndio walioyafanya.

 Mauaji ya Mpeketo yemesababisha vifo vya watu zaidi ya hamsini.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema mauaji yaliyofanywa katika mji wa Mpeketoni, Pwani ya Kenya hayakufanywa na kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Al Shabaab.

Katika taarifa yake Rais Kenyatta kupitia televisheni siku moja baada ya kundi hilo kukiri kufanya mauaji yaliyotokea Mpeketoni Jumapili usiku, amesema hakuna ushahidi unaothibitisha kuwa shambulizi hilo lilitekelezwa na Al Shabab bali hata wanasiasa walihusika.

Kundi la Al Shabaab lenyewe lilikiri kupitia vyombo vya habari kuwa ndilo lililofanya mauaji hayo.

Rais Kenyatta amesema maafisa waliohusika tayari wameachishwa kazi na kwamba watashitakiwa na kuongeza kuwa bado wanaendelea kuwanachunguza wanasiasa waliohusika na mauaji hayo.

Mauaji mengine yamefanyika usiku wa kuamkia leo licha ya taarifa ya Al Shabaab kusema kuwa washambuliaji walioshambulia Mpeketo walikuwa wamerejea salama nchini Somalia.

Uharibifu mkubwa ulishuhudiwa katika mji huo huku washambuliaji wakichoma hoteli na kituo cha polisi pamoja na kuteketeza magari waliyoyatumia kwa usafiri wao.
Kenyatta amesema kuwa kuna baadhi ya wanasiasa wanaochochea uhasama miongoni mwa jamii.

Post a Comment

 
Top