Rais wa Marekani Barack Obama ameliambia bunge kuwa Marekani inawapeleka wanajeshi wake 275 kwenda kutoa msaada na kuweka usalama kwa wafanyakazi wa Marekani na ubalozi wake mjini Baghdad, Iraq.

Hatua hiyo inakuja baada ya wanamgambo wa jihadi kuidhibiti sehemu kubwa ya kaskazini mwa Iraq katika operesheni kali iliyofanywa wiki iliyopita na kuitwaa miji kadhaa ukiwemo mji wa pili kwa ukubwa nchini humo, Mosul.

Obama amesema katika barua iliyotumwa kwa wabunge kuwa jeshi la Marekani linaelekea Iraq ili kuwalinda raia wa Marekani pamoja na mali ya nchi, na litapewa uwezo wa kuwa tayari kupambana kwenye vita.

Rais Obama amesema amelifahamisha bunge chini ya Sheria ya Mamlaka ya Kivita, maana kuwa uamuzi huo unaweza kutolewa bila kupigiwa kura bungeni.

Post a Comment

 
Top