Hivi karibuni tu kumekuwa kukiripotiwa kuwepo kwa mautukio tofauti ya unyanyasaji akiwemo Marehemu mtoto Nasra Mohamed kule Morogoro, lakini bado jamii haijalichukua hilo kama funzo badala yake wapo ambao wanendeleza unyanyasaji kwa watoto wao.

Kijana Yusto Kikoti mkazi wa kijiji cha Mkoga manispaa ya iringa mwenye umri wa miaka 19 ameunguzwa na mchuzi wa nyama na mama yake mzazi Sophia Kikoti kwa kile kinachodaiwa kuwa eti aliunguza nyama jikoni ambayo aliachiwa apike.

Siku ya tukio mama mzazi alimuaga mawanae kuwa anaelekea Ruaha mtoni kuteka maji na kumwachia chungu cha mboga achochee pamoja na mapipa ya pombe ya kienyeji na kumtaka mwanae aendelee kuchochea ndipo kijana huyo alipojisahau mpaka mboga kuungulia.

Mama huyo mara baada ya kurejea kutoka mtoni na kung'amua kilichofanyika kwa hasira akaamua kuchota mchuzi wa nyama iliyokuwa ikiendelea kuiva motoni na kumwagia mwilini kijana huyo na kumsababishia maumivi makali na michubuko. 

Yusto ambaye ni mwanafunzi wa chuo cha St. Tereza anayesomea fani ya ufundi seremala ambaye kwa mujibu wa maelezo yake amesema siku hiyo yeye alikuwa likizo na kuamua kurejea nyumbani ili kumsaidia kazi za mavuno mama yake mzazi na kukutana na kisanga hicho.

Ndugu wa mtoto huyo akiwemo mjomba wake walikutwa uchungu na kuamua kumsaidia kijana huyo kumpeleka hospitali kwaajili ya matibabu.

Katika mahojiano na mama huyo ambaye awali hakutaka kutoa maelezo na kuonesha ubabe akaamua kufunguka na kusema kuwa hizo zilikuwa ni hasira tu na kuonesha hali ya kuto kujali alichokifanya na kuendelea kutoa majibu ya jeuri.

Mwenyekiti wa kijiji hicho Hamis Luhanga alipofikishiwa taarifa hizi akatuma mgambo na kumuweka chini ya ulinzi mtuhumiwa na kisha kupelekwa polisi.






 Mama mzazi wa mtoto wa kijana Yusto akiwa chini ya ulinzi nyumbani kwa mwenyekiti.
Mama na kijana huyo akipelekwa polisi.

Post a Comment

 
Top