Kubomolewa kwa Daraja la Solodela linalounganisha kata ya Ilembula na Luduga wilayani Wanging'ombe mkoani Njombe kumepelekea ugumu wa shughuli za usafirishaji wa bidhaa ndani ya halmashauri hiyo.

Daraja hilo ambalo limebomolewa kwa minajili ya kutanuliwa lakini kwa muda wa takribani miezi minne mfululizo bila kufanyika marekebisho yoyote mpangu uliotarajiwa kukamilika katika kipindi cha kiangazi lakini mpaka msimu wa mvua ujenzi haujafanyika.

Magari na wasafiri wanalazimika kuzunguka barabara ya Igando-Njombe.
 Daraja lililotengenezwa kwa muda ambalo halina uwezo wa kupitisha magari ya mizigo na abiria na likinyeshewa hakuna gari linalopita.


 Gari ndogo ikijaribu kupita eneo hilo kwa tabu.
 Daraja lililobomolewa ambalo awali lilikuwa na uwezo wa kupitisha gari moja tu.

Post a Comment

 
Top