Kundi la wapiganaji wa Al Shabaab
nchini Somalia, limekiri kufanya mashambulizi katika eneo la Mpeketoni karibu
na Lamu, Pwani ya Kenya na kusababisha vifo vya watu takriban 49 huku wakikiri kuwa
shambulizi hilo wametoa onyo kwa watalii kukoma kuja Kenya.
Taarifa ya kundi hilo ilisema kuwa
shambulizi hilo lilikuwa la kulipiza kisasi dhidi ya serikali ya Kenya kwa
kufanya msako dhidi ya waisilamu kwa njia ya kuwafunga kiholela na kuwaua
wahubiri wa kiisilamu.
Baadhi ya walioshuhudia mashambulizi
hayo wamearifu BBC kuwa wameona maiti kadhaa na majeruhi wengi japo Polisi
hawajathibitisha ni watu wangapi wameuawa.
Mji wa Mpeketoni uko umbali wa
kilomita miamoja kutoka eneo la mpakani na SomaliaKenya imekumbwa na mashambulio
kadhaa kutoka kwa wapiganaji wa kisomali wa Al Shabaab tangu ipeleke wanajeshi
wake Somalia mwaka wa 2011.
Wapiganaji hao walifika katika
malori mawili na kurusha kifaa kama bomu ndani ya kituo cha polisi kisha
wakakivamia na kuiba silaha na kuteketeza hoteli na vijiji huku wakiwapiga watu
risasi kiholela.
BBC- Swahili
Post a Comment