Mwanafunzi ambaye amefahamika kwa jina moja la LEMA Alikua akisoma mwaka wa 4 kozi ya sheria katika chuo kikuu kishiriki cha Mt.Augustino Tawi la Iringa (Ruaha University College-RUCO), mwanzoni mwa wiki hii ameshambuliwa kwa kuunguzwa na moto akidhaniwa ni mwizi.

Mnamo tarehe 24.06.2014 mwanafunzi huyo alikua ametoka kuangalia michuano ya kombe la dunia na akiwa amelewa akawa anatafuta chakula cha jioni na ilikua majira ya saa 5 Usiku, Mwanafunzi huyo aliingia kwenye mgahawa ambao biashara ilikua imefungwa kwa muda huo lakini ndani kulikuwapo na binti ambaye alianza kupiga kelele kwa kudhani alikua mwizi.

Na kwakua eneo hilo kulikuwa na mlinzi(Mmasai) ndiye aliyeanza kumshambulia mwanafunzi huyo.

Baada ya tukio hilo wakatokea watu  (2) waliojitambulisha kuwa ni askari wakaamuru mwanafunzi huyo asipigwe kwa madai ya kumfikisha kituoni.

Lakini baada ya mwendo mfupi kuelekea kituoni mwananchi mmoja alimchukua kijana huyo kinguvu kisha kumwagia mafuta na kisha kumuwasha moto, ambao ulizimwa na madereva bodabora walio kuwa eneo hilo na kisha kumkumbiza kijana huyo hospitali.

Mpaka sasa Kijana huyo amelazwa katika wodi ya watu mahututi (ICU) katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa ambapo mama yake mzazi pamoja na kaka yake ndio wanaomsaidia kumuhudumia.

Post a Comment

 
Top