Wakati wakishuka tayari kwa kuonesha kombe hilo
umati wa washabiki wa kandanda wa Ujerumani wamejitokeza katika mitaa mbalimbali ya
jiji la Berlin kuilaki Timu yao ya Taifa ambayo juzi ilinyakua kombe la Dunia
kwa mara ya nne.
Wengi
walianza kujikusanya kabla hata ya mawio wakiisubiri timu yao iliyokuwa
ikitokea Rio de Janeiro, asubuhi ya leo Jumanne.
Umati
mkubwa ulijitokeza na kujikusanya kandakando ya barabara za jiji hilo kushuhudia
timu yao ikipita katika mitaa yao kwa kutumia gari maalumu.
Shamrashamra
kubwa zimefanyika katika lango la Brandenburg, ambako wachezaji wameonesha kombe
hilo ambalo kwa mara ya mwisho walilitwaa mwaka 1990.
Katika
fainali zilizoacha kilio kikubwa kwa waliokuwa wenyeji wa michuano hiyo Brazil,
Ujerumani ilifanikiwa kurudi na kombe hilo la dhahabu baada ya kuinyuka timu
ngumu ya Argentina kwa bao 1-0.
Ushindi
huo unaifanya Ujerumani iwe imeshinda michuano hiyo mikubwa kuliko yote duniani
kwa mara ya nne sasa. Miaka mingine ikiwa ni 1954, 1974 na 1990.
Post a Comment