Je ni kweli wake wanaponenepa upita kiasi ndio sababu ya waume zao kuwa na mipango ya kando?
Nchini Kenya mjadala umezuka kwenye mitandao ya
kijamii kufuatia maandishi ya mwanamke mmoja akiwalaumu wanawake wanene
kupita kiasi kwa masaibu yanayowakumba katika ndoa zao.Amesema wanawake wanapoolewa na kubarikiwa na watoto , unene huzuka na hapa ndipo Njoki anasema pindi mwanamke anapoonza kunenepa na kuwa mzito kupita kiasi, waume zao husasau yule kidosho aliyemfumba macho hata akamuoa.
Anaongeza kusema wanawake hao huzua kila sababu kutofanya mazoezi na wakisema wana shughuli nyingi.
Kadhalika anasema wanawake hujipatia majukumu mengi na kujishughulisha kiasi cha kujisahahu. Wao husema unene umetokana na kupata mtoto lakini kwa Njoki, hicho ni kisingizio tu.
Waume zao wanapotupa jicho huku na kule na kujionea wasichana walio na umbo zuri basi huingia kwenye mtego wa kujiingiza katika zinaa.
Matamshi ya Njoki yamewakera wengi hasa wanawake na kuzua hisia mseto miongoni mwa watu wengi. Bila shaka aliandika maoni yake na sisi tunakuuliza tu maoni yako.
Kwa nini swala hili la unene na wembamba ndilo linatumiwa kama kigezo kwa wanaume waliooa kwenda nje ya ndoa?
Je unahisi kama kuna ukweli hapa au Njoki ana matatizo yake mwenyewe? Yeye mwenyewe ni mwembamba.
Post a Comment