Bi Mugabe ameteuliwa kuongoza kitengo cha wanawake katika ZANU-PF.

Mkewe rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ameingia katika uongozi wa chama tawala cha Zanu-PF .
Grace 49 ameteuliwa kuongoza kitengo cha wanawake cha Zanu -PF ,wadhfa atakaochukuwa rasmi mwezi Desemba katika kongamano la kitaifa la wanachama wa ZANU-PF.

Mwandishi wa BBC aliyeko mjini Harare Brian Hungwe anasema cheo hicho kitamruhusu Bi Mugabe kushiriki katika mikutano ya kamati kuu ya chama hicho ambayo ni yenye shinikizo kubwa katika uendeshaji wa taifa hilo la kusini mwa Afrika.

Kumekuwa na mvutano na taharuki kubwa katika chama cha Zanu-PF kufuatia kuzorota kwa Afya ya rais Mugabe katika miaka ya hivi karibuni na haijulikana ni nani atakayemrithi kiongozi huyo wa Zimbabwe.
Bi Grace ni mke wa pili wa rais Robert Mugabe.

Bi Mugabe atahudumu kama katibu mkuu wa kitengo cha wanawake baada ya kuteuliwa katika mkutano wa kamati kuu iliyofanyika mjini Harare.

Bi Mugabe alikuwa wakati mmoja msaidizi wake rais Mugabe kabla hawajoana mwaka wa 1996.
Wamejaliwa watoto watatu.

Rais Mugabe 90,alihudhuria kikao hicho .
Bwana Mugabe ametawalataifa hilo tangu itwae uhuru wake mwaka wa 1980.
BBC-Swahili

Post a Comment

 
Top