Picha ya marehemu Ibrahim Faraja Chipungahelo enzi za uhai wake.

Tukio la mtoto wa umri wa miaka 9 kuuawa na kisha kuliwa na mbwa lililotokea hivi karibuni wilayani Ludewa Mkoani Njombe lilizua taflani mara baada ya kusambaa kwa taarifa kuwa mmiliki wa mbwa hao ametishia kuwachukulia hatua za kisheria wananchi ambao walishikwa na hasira kisha kuwaua mbwa wake.

Wananchi hao wakishirikiana na ndugu wa marehemu mara baada ya kifo na ndugu yao waliandamana mpaka nyumbani kwa mmiliki wa mbwa hao ambaye kwa muda huo hakuwepo kisha kuwatoa mbwa wote waliokuwa bandani kisha kuwashambulia kwa kuwapiga na kuwaua.

Hali ya hewa ilichafuka katika mji wa Ludewa baada ya kuvuma kwa taarifa za vitisho toka kwa mmiliki wa mbwa anayefahamika kwa jina la Bosco lingalangala kuwa alitaka kuwaadhibu waliotekeleza shambulio hilo ndipo Ebony fm imemtafuta Bosco na kutaka kufahama busara yake katika hilo ambaye amekanusha uvumi huo.

Kuhusiana na suala la kuwashitaki wananchi walohusika kuwaua mbwa wake na kisha kuwachoma moto, Bosco amebainisha kuwa kwa sasa anashughulika na msiba kwanza na taratibu nyingine zitafuatwa baadae.

Diwani wa kata ya Ludewa Monica Mchilo ameonesha  hali ya kutoridhishwa  na kauli za mmiliki wa mbwa hao yakutaka kuwashtaki wananchi  walio waua mbwa wake.

Hata hivyo mkuu wa wilaya ya Ludewa Juma Solomon Madaha amesema  wakati tukio hilo linatokea  yeye alikuwa safarini Mkoani Mtwara na sasa yuko Dodoma kikazi , na kudai kuwa kikubwa ni mmiliki wa mbwa hao kuomba radhi wazazi na jamii  ya wilaya ya Ludewa  na kusisitiza kuwa  sheria  lazima ichukue mkondo wake.

Mwanafunzi Ibrahim Chipungahelo aliyekuwa mwanafunzi wa shule ya msingi Ludewa mjini aliuawa na Mbwa August 8 mwaka huu majira ya mchana katika eneo la Ikulu wilayani Ludewa  akiwa njiani pamoja na wenzake wakati wakirejea makwao.

  Jeneza ambalo mwili wa Ibrahim ulihiofadhiwa.
Wananchi walioandamana kuhakikisha Mbwa hao wanauaw.

Post a Comment

 
Top