Rais Barack Obama.
Rais Barack Obama wa Marekani ameidhinisha kupelekwa
vikosi vya wanajeshi wapatao 350 kwa lengo la kuwalinda wanadiplomasia
na wafanyakazi raia wa nchi hiyo waishio mji mkuu wa Iraq Baghdad.
Hata hivyo Marekani inatarajia kuwatuma maofisa waandamizi akiwemo John kerry katibu mkuu wa marekani na Chuck Hagel katibu wa ulinzi ambao watakwenda mashariki ya kati katika harakati za kuimarisha ushirikiano.
Hatua hiyo inafuatia vitendo vya mashambulizi na mauaji yanayoendelea Iraq ikiwa ni matokeo ya utofauti kati ya Marekani na makundi ya wapiganaji ambao wamekuwa wakiwalenga raia wa Marekani waliopo nchini humo.
BBC-Swahili.
Post a Comment