Wanajeshi 12 wahukumiwa kifo kwa kukiuka kanuni za jeshi.

Wanajeshi kumi na wawili nchini Nigeria wamepewa adhabu ya kifo kwa uasi pamoja na jaribio la mauji.

Hii ni baada ya kumfyatuliwa bunduki afisa mkuu anayeongoza operesheni ya kupambana dhidi ya kundi haramu la kiislamu la Boko Haram kati mji wa Maiduguri,kaskazini Mashariki mwa nchi, mwezi wa Mei.

Wanajeshi wengine watano waliachiliwa baada ya ushahidi kukosekana.

Wanajeshi hao 12 walipatikana na hatia ya kumfyatulia risasi Jemedari amadu Mohammed.
Wanajeshi hao walikasirishwa na kamanda wao ambaye walimlaumu kwa kukataa kuchukua hatua baada ya msafara wao kushambuliwa.

Jeshi la Nigeria limeshindwa kuwashinda Boko Haram na wanajeshi wamekuwa wakilalamika kuwa kila wanapokabiliana na wapiganaji wa Boko Haram hawana silaha za kutosha kukabiliana nao.
Wote walikana mashtaka hayo katika Mahakama ya kijeshi mjini Abuja.
Mahakama ya kijeshi ya watu tisa ilisikiza kuwa tukio hilo lilitendeka baada ya kufyatuliwa kwa risasi kwa afisa mkuu wa kitengocha 7 cha jeshi la Nigeria.
 Kitengo hicho cha Jeshi ndicho kinakabiliana na Boko Haram.
Ilimbidi Generali Amadu Mohammed kujificha walipomlenga na bunduki zao.
Hata hivyo, hakuumia.

Kiongozi wa mahakama Chukwuemeka Okonkwoalisema kuwa hata kama hukumu hizi zilikuwa chini ya udhibitisho wa mamlaka ya jeshi la Nigeria, hakukuwa na shaka juu ya uzito wa kosa hilo.

Mwezi uliyopita, kundi la wanajeshi kaskazini masharikimwa Nigeria walikataa kupambana na Boko Haram mpaka wapatiwe vifaa bora, mmoja wao aliiambia BBC.
BBC-Swahili.

Post a Comment

 
Top