Jeshi La Polisi Mkoa Wa Njombe Linawashikilia Watu 12  Wanaosadikika Kuwa Ni Majambazi  Sugu  Wa Kutumia Silaha za moto Ambao Wamekamatwa Katika Oparesheni Iliyofanyika Kwa Kipindi  Cha Siku Mbili Kutoka Octoba 1 hadi 2 Mwaka Huu  Katika Maeneo Mbalimbali mkoani humo.

Akizungumza Na Waandishi Wa Habari Pamoja Na Wamiliki Wa Mali  Zilizokamatwa  Kwenye Msako Huo Kamanda Wa Jeshi La Polisi Mkoa Wa Njombe SACP  Fulgence Ngonyani  Amesema Watuhumiwa Hao    Wamekamatwa Kwa Makosa  Mbalimbali Ikiwemo Uvunjaji,Kupatikana Na Silaha,Kucheza Kamali,Wizi Wa Mifugo Na  Kukutwa Na Mali Mbalimbali  Ambazo Zinadhaniwa kuwa Ni Za Wizi.

Kamanda Ngonyani Amewataja Watuhumiwa Wanne Waliokamatwa Na Silaha Aina Ya Bastola  Iliyotengenezwa Kienyeji Na Risasi Mbili Za Bunduki aina ya Short Gun  Na Wizi Wa Mifugo Kuwa Ni Shukuru Lugenge Mweye Umri Wa Miaka 42 ,Abdul Kaduma Mwenye Miaka 38  ,Rashidi mguruni  Mwenye Miaka 28  Na Gervas Muhuti Mwenye Umri Wa Miaka 50   Wakazi  Wa  Katenge Na Maguvani Katika Halmashauri Ya Mji Wa Makambako Mkoani Njombe.

Ngonyani Amesema  Watuhumiwa Wengine Waliokamatwa Na Mali Za Wizi  Ni Pamoja Na   Salumu Hongori Mkazi Wa Mgendela,Peter Matola Na,Joshua Mwalongo Wakazi Wa Mjimwema,Eva Kawogo Mkazi Wa Nationalhousing ,Issa Shaban Mkazi Wa Uzunguni, Emili Mwalongo Mkazi Wa  Nazareth,Peter Luiva Mkazi Wa National Housing Na Salumu Kawogo Wote Wakazi Wa  Njombe Mjini.

Badhi Ya Wamiliki Waliofika Katika Ofisi Za Jeshi La Polisi Wamelipongeza Jeshi la polisi kwa jitihada hizo na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano licha ya baadhi yao kushindwa kuziona Mali Walizo Wahi Kuibiwa  Na Wengine Wakifanikiwa Kuzitambua.

Aidha Kamanda Ngonyani Amesema Kuwa  Watuhumiwa Hao Wote Watafikishwa  Mahakamani Kujibu Tuhuma Zinazowakabili Ambapo Ametoa Wito Kwa Wananchi  Waliowahi Kuibiwa Kufika Katika Ofisi Za Jeshi La Polisi Mkoa Wa Njombe Ili Kuweza  Kutambua Mali Zao.

Post a Comment

 
Top