Keneth Mwangoka (Msanifu) akionesha kiwango cha ubunifu katika utengenezaji wa gari hilo, mradi unaomwingizia kipato.
 Mwana habari na Riporter wa Ebony fm na Stear tv Oliver Motto anaye onesha kupigwa na butwaa kuliona gari hilo macho mwake.
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Peter Tweve akimpongeza Mwangoka kwa ubinifu huo.
Kenny Mwangoka akiendesha gari hilo ambalo bodi lake limetengenezwa kwa mbao

 HUWEZI KUAMINI, lakini huo ndio ukweli. Bodi la gari hili aina ya Hiace lenye namba za usajili T921 BME limetengenezwa kwa mbao aina ya mlingoti na pine.

Gari hili linamilikiwa na mvunaji na mfanyabishara wa mbao katika kijiji cha Nyololo, wilayani Mufindi Kenny Mwangoka.

Jitihada za Mwangoka kulifufua gari hilo kwa kuvisha bodi mpya hazikuzaa matunda na ndipo alipotumia ubunifu huu.

"Mimi mwenyewe ni fundi wa magari, kwahiyo kazi ya kuunda na kuvisha bodi hili la mbao nilifanya mwenyewe," anasema.

Anasema baada ya matengenezo hayo gari hilo limekuwa kivutio kikubwa sehemu mbalimbali anazopita nalo.

"Sasa nalitumia kuhamasisha utalii, hasa utalii wa mazingira nikiwa na maana kwamba tukiyatunza mazingira yatatufaa kwa mambo mengi ikiwa ni pamoja na matengenezo ya magari kama hili langu," anasema.

Anasema gari hilo atalipeleka kwenye maonesho ya nanenane kama moja ya njia za kuhamasisha upandaji wa miti. 


Lakini mbali na hayo Kenny hakuishia hapo tu kwani aliigeukia serikali kwa kutothamini michango wa wasanifu kama hawa badala yake viongozi wako mbio kuwakandamiza na kuwataka kulipia mapato makubwa hadi kufikia kufifisha jitihada.

Post a Comment

 
Top