NA HII NI ZAIDI YA DARASA:UALIMU NI WITO ILA WATANZANIA TUMESAHAU?
Hakika ulimwenguni kuna mengi ya kujifunza…….
Wakati waalimu nchini Tanzania wamekuwa wakilalamika kufanya kazi katika mazingira magumu na kuizonga serikali waki dai haki zao, huko barani ASIA katika moja YA vijiji kumeripotiwa kuwepo kwa mwalimu mmoja ambaye yeye hana usafiri wa kwenda kazini na hutembea umbali mrefu kila siku ili kufika kazini kwake….
Lakini kama haitoshi ili kufika shuleni hapo mwalimu huyo amekuwa akilazimika kuvuka mto kwa kuogelea kwa kuwa hakuna miundo mbinu ya kumsaidia kuvuka….
Mwalimu huyo hutembea na nguo za kubadili katika mfuko wake wa rambo na mara baada ya kufika shuleni ndipo hubadili nguo zake na kuendelea na kazi na wakati wa kurudi zoezi hilo pia hufanyika.....
Na huenda ule usemi wa ualimu ni wito ukawa ndio unamfanya ayatimize hayo tofauti na waalimu wa Tanzania......
Na waweza tembelea www.ebony fm radio kuona picha za mwalimu huyo akiogelea kuvuka mto huku akiwa na mfuko wa rambo....
Post a Comment