Tunaomba radhi kwa picha hii.

Wanamgambo wa Kikristo nchini Afrika ya kati wamewaua vijana watatu Waislamu na kukatakata viungo vyao vya mwili mjini Bangui wakati walipokuwa wakijitayarisha kwenda kutazama mechi ya mpira.

Mechi hiyo ilikuwa baina ya vijana Waislamu na Wakristo kwa lengo la kuleta amani na maelewano baina ya Waislamu wa kundi la Seleka na wanagamabo wa Kikrsito wa kundi la Anti Balaka.

Miili ya vijana hao waliokuwa wakazi wa mtaa wa PK5 katika mji mkuu wa nchi hiyo Bangui imezikwa katika msikiti mmoja mjini humo.

Msemaji wa kundi la Kikristo la Anti-Balaka Sebastien Wenezoui amedai kulaani mauaji hayo na kuongeza kuwa vijana wengine 10 Waislamu wametekwa nyara katika tukio hilo.
 
Siku ya Jumamosi kuliripotiwa mapigano makali baina ya wanajeshi wa Ufaransa na Waislamu watiifu kwa kundi la Seleka katika mji wa Bambari.

Wanajeshi wa Ufaransa wajulikanao kama Sangaris wamekuwa wakiwashambulia Waislamu na kupuuza ugaidi unaofanywa na wanamgambo wa Kikristo.
Radio Tehran.

Post a Comment

 
Top