Wapiganaji wa Al Shabaab

Serikali ya Kenya imethibitisha kuwa maafisa wake wawili wa jeshi wameuawa na wengine wawili kujeruhiwa, baada ya wapiganaji wa Kiislamu wa Al Shaabab kufanya shambulio la kuvizia, baada magari yao kukwama barabarani huko nchini Somalia.

Ripoti zinasema msafara wa wanajeshi wa Kenya ulikuwa ukielekea eneo la Ras Kamboni wakati shambulio hilo lilipotokea.

Kwa upande wao, msemaji wa Al shabaab, Abu Mus'ab amedai kuwa wapiganaji wake walifanikiwa kuteketeza magari kadhaa ya jeshi la Kenya, madai ambayo yamekanushwa vikali na utawala nchini kenya.

Aidha amesema wapiganaji kadhaa wa Al shabaab waliuawa na wengine kujeruhiwa wakati wa makabiliano hayo.
Radio Tehran.

Post a Comment

 
Top