Wananchi katika eneo la Mlandege manispaa ya Iringa mwishoni mwa wiki iliyopita walichukua hatua ya kufunga barabara iliyopo mkabala na shule ya msingi Mshikamano wakiishinikisha serikali kuondoa taka zilizorundikana katika eneo hilo kwa muda wa zaidi ya miezi mitatu.
Asubuhi vijana wa eneo hilo waliwazuia akina mama waliokuwa wakitaka kutupa taka katika dampo lililopo maeneo hayo na kuwaamuru wazimwage barabarani.
Mpaka majira ya saa nne asubuhi tayari kuliwa na mrundikano wa taka katikati ya barabara hiyo inayoelekea nyumbani kwa Mstahiki Meya wa manispaa ya Iringa Amani Mwamwindi, huku wakazi wa eneo hilo wakionesha msimamo wa kutaka guba kurudishwa tena eneo hilo.
Kwa mujibu wa maelezo ya wakazi wa eneo hilo, ni kwamba awali kulikuwepo na guba (Pipa) la taka katika eneo hilo lakini tangu lilipo ondolewa na manispaa yenyewe mwezi Januari mwaka huu halikurudishwa, na kuwalazimu wakazi kuendelea kumwaga taka chini ambazo mpaka sasa kutokana na hali iliyopo huenda kukatokea milipuko ya magonjwa kwani eneo lina harufu mbaya na wadudu wengi mno.
Asubuhi hiyo Ebony fm kupitia kipindi chake cha Morning Talk ilimtafuta Meya ambaye alikiri kupokea malalamoko na kwa lugha nyepesi kabisa akaahidi kulichukua kama changamoto na kulifanyia kazi.
Post a Comment