Walimu nchini Nigeria wanafanya maandamano ya siku
moja kushinikiza serikali kuharakisha juhudi zake za kuwatafuta
wasichana waliotekwa nyara na kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Boko
Haram zaidi ya mwezi mmoja uliopita.
Kiongozi mmoja wa walimu hao aliambia BBC kwamba zaidi ya walimu miamoja sabini wameuawa mwaka huu.
Alituhumu maafisa wa serikali kwa kutoongeza juhudi za kuwalinda walimu na badala yake kujihusisha zaidi na siasa.
Wakati huohuo, Marekani imetuma vikosi vyake nchini Chad , nchi ambayo inapakana na Nigeria kama sehemu za juhudi zake kusaidia katika kuwatafuta wasichana waliotekwa nyara.
Post a Comment