Watu wanaotazama runinga kwa saa tatu au zaidi kila
siku wako katika hatari ya kuaga dunia mapema kuwaliko wale wanaotazama
kwa muda mchache.
“Matokeo ya utafiti wetu ni sambamba na utafiti tuliowahi kufanya, ambapo muda unaotumiwa kutazama runinga uliolinganishwa na idadi ya vifo vinavyotokea kwa sababu hiyo.”
Watafiti hao waliwachunguz vijana wachanga 13,284 kutoka Uhispania wenye afya na waliohitimu chuo kikuu kuhusu aina tatu ya tabia za kukaa tu na hatari ya kuaga dunia kutokana na sababu zote:muda wa kutazama runinga, muda wa kutumia tarakilishi na muda wa kuendesha gari.
'Sababu nyinginezo'
Vijana hao walioshiriki, ambao walikuwa na umri wa wastani wa miaka 37 na ambao asilimia 67 walikuwa wanawake, walifuatiliwa kwa takriban miaka 8.2. mwishowe, vifo 97 viliripotiwa, vikiwemo vifo 19 vilivyotokana na mishipa na moyo, 46 kutokana na saratani na mengine 32 vilivyotokana na sababu nyinginezo.
Utafiti huo ulionyesha hatari kubwa ya kuaga dunia ilikuwa mara mbili zaidi kwa washiriki walioripoti kutazama runinga kwa saa tatu au zaidi kwa siku ikilinganishwa na wale waliotazama kwa saa moja au chini ya saa.
Watu 19 waliripotiwa kufariki kutokana na kutizama TV kwa muda mrefu.
Hatari hii mara mbili zaidi ilidhihirishwa pia baada ya kutoa hesabu ya safu kubwa ya vigezo vingine vinavyohusiana na hatari kubwa ya kuaga dunia.
Watafiti hao hawakupata ushirikiano kati ya muda unaotumiwa na mtu anapotumia tarakilishi au kuendesha gari na hatari kubwa ya kuaga dunia mapema kutokana na sababu zote.
Pia waliongezea kuwa utafiti zaidi unapaswa kufanywa ili kudhibitisha ni athari zipi zilizopo kati ya kutumia tarakilishi na kuendesha gari katika viwango vya vifo, na pia kutathmini taratibu za kibayolojia zinazoweza kueleza uhusiano huo.
“Watu wanapoendelea kuzeeka, tabia za kukaa tu zitaenea zaidi, hasa kutazama runinga, na hili litasababisha mzigo mkubwa katika ongezeko la matatizo ya kiafya yanayoambatana na kuzeeka,” Martinez-Gonzalez alisema.
“Matokeo ya utafiti wetu yanapendekeza watu wazima wajihusishe katika mazoezi ya viungo, waache kukaa tu kwa muda mrefu, na wapunguze kutazama televisheni kwa zaidi ya saa mbili kila siku.”
BBC-Swahili.
Post a Comment