Mwili wa Daniel Lema ukiagwa na baadhi ya wanachuo pamoja na raia waliojitokeza kuhudhuria ibada ya kuuaga mwili wa marehemu mapema asubuhi ya leo katika hospitali ya rufaa mkoani iringa.
Baadhi ya raia walijitokeza kumuaga Lema katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya rufaa mkoani Iringa.
LEMA Aliyekua akisoma mwaka
wa 4 kozi ya sheria katika chuo kikuu kishiriki cha Mt.Augustino Tawi
la Iringa (Ruaha University College-RUCO), mwanzoni mwa wiki hii ameshambuliwa kwa kuunguzwa na moto akidhaniwa ni mwizi.
Mnamo tarehe 24.06.2014
mwanafunzi huyo alikua ametoka kuangalia michuano ya kombe la dunia na
akiwa amelewa akawa anatafuta chakula cha jioni na ilikua majira ya saa 5
Usiku, Mwanafunzi huyo aliingia kwenye mgahawa ambao biashara ilikua
imefungwa kwa muda huo lakini ndani kulikuwapo na binti ambaye alianza
kupiga kelele kwa kudhani alikua mwizi.
Na kwakua eneo hilo kulikuwa na
mlinzi(Mmasai) ndiye aliyeanza kumshambulia mwanafunzi huyo.
Baada ya tukio hilo wakatokea watu (2) waliojitambulisha kuwa ni askari
wakaamuru mwanafunzi huyo asipigwe kwa madai ya kumfikisha kituoni.
Lakini baada ya mwendo mfupi kuelekea kituoni mwananchi mmoja alimchukua
kijana huyo kinguvu kisha kumwagia mafuta na kisha kumuwasha moto,
ambao ulizimwa na madereva bodabora walio kuwa eneo hilo na kisha
kumkumbiza kijana huyo hospitali.
Mpaka sasa Kijana huyo amelazwa katika wodi ya watu mahututi (ICU)
katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa ambapo mama yake mzazi
pamoja na kaka yake ndio wanaomsaidia kumuhudumia.
Mwili wake umeagwa mapema leo katika hospitali ya rufaa mkoani Iringa tayari kwa safari ya kuelekea mkoani Kilimanjaro kwaajili ya mazishi yatakayofanyika siku ya juma tano.
Lema alizaliwa mnamo tarehe 05/06/1989 na kufariki tarehe 30/06/2014 Mungu na ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi!!!
Home
»
»Unlabelled
» SAFARI YA MWISHO YA MWANAFUNZI DANIEL LEMA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment