Kumetokea shambulizi la bomu mbele ya soko lenye shughuli nyingi katika mji mkuu wa Nigeria Abuja na kuwauwa zaidi ya watu 21.

Taswira ya majonzi na kilio imetanda katika mji wa Abuja, mamia ya watu waliokuwa wakinunua bidhaa katika soko hilo wakijikuta wakivuja damu kutokana na majeraha ya mlipuko huo na wengine kuishia mauti.
Bomu hilo limelipuka mbele ya kituo kikubwa cha biashara, kinachotembelewa na watu wengi ambapo Magari yamechomwa kabisa na vioo katika madirisha ya nyumba zilizokuwa karibu kuvunjika vyote.

Lakini Serikali ya Nigeria imesema kuwa hakuna ushahidi kuwa utekaji nyara ulitendeka. Serikali ilisema vivyo hivyo wakati zaidi ya wasichana wanafunzi zaidi ya 200 walitekwa nyara na Boko Haram mnamo Aprili.

Wachunguzi wengi wanasema kuwa kwa kukanusha kuwa kuna utovu wa usalama nchini Nigeria, Serikali imechanganyikiwa kwa sababu milipuko ya mabomu ya mara kwa mara ni ushahidi tosha kuwa ukosefu wa usalama ndio ukweli wa mambo nchini.

Post a Comment

 
Top