Zaidi ya Watanzania 50 wamehukumiwa adhabu ya kifo nchini China baada ya kupatikana na hatia ya kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya.

Idadi hiyo ni kati ya Watanzania 403 wanaoshikiliwa katika nchi mbalimbali kwa tuhuma hizo.

Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,uratibu na Bunge nchini humo,William Lukuvi ametaja baadhi ya nchi ambazo Watanzania wanashikiliwa kuwa Kenya,Uganda,Botswana,Malawi,Msumbiji, China,Brazil,Marekani,Pakistani na Uturuki.

Serikali ya Tanzania imekamilisha muswada wa sheria ya dawa za kulevya ambao ikiwa utapitishwa bungeni utasaidia harakati za kupambana na biashara ya dawa za kulevya.

kwa mujibu wa Lukuvi, kuanzia mwezi Januari mpaka juni mwaka huu,kiasi cha kilo 220 za dawa za kulevya aina ya Heroine na watuhumiwa 18 walikamatwa pia kilo 15.4 za Cocaine zilikamatwa sambamba na watuhumiwa saba.
BBC-Swahili.

Post a Comment

 
Top