Taarifa kutoka nchini Sudan zinasema kuwa mwanamke aliyeachiliwa hapo jana kwa kosa la kuasi dini ya kiislamu amekamatwa tena.
Duru zinasema kuwa Meriam Ibrahim aliyejifungulia jela alikuwa anajiandaa kuondoka nchini Sudan pamoja na familia yake.
Haijulikani kwa nini alikamatwa na karibu watu 40 waliokuwa wamevalia mavazi ya kiraia siku moja tu baada ya kuachiliwa kuambatana na uamuzi wa mahakama ya rufaa.
Meriam alikamatwa kwa mara ya kwanza mwezi Februari na kujifungulia mtoto wake msichana jela baada ya kuhukumiwa.
Mwana mama huyo alikamatwa mara ya kwanza mwezi Februari na kujifungulia mtoto wake msichana jela punde baada ya kuhukumiwa.
Familia yake imepelekwa katika makao makuu ya idara ya ujasusi.
Kabla ya kuzuiliwa kwake tena, jamii ya kimataifa ilipongeza uamuzi wa kuachiliwa kwake na kumuondolea hukumu ya kifo chake.
Post a Comment