Vitendo vya kikatili bado vinaendelea kuripotiwa mjini Iringa ambapo leo mwili wa mtoto mchanga anayekadiriwa kuwa na umri wa miezi 7 umeokotwa ukiwa umetupwa ndani ya dampo la taka katikati ya manispaa ya iringa eneo la mnara wa saa barabara iendayo katika ofisi za mkuu wa wilaya ya Iringa vijijini.

Mtoto huyo ambaye anakadiriwa kuwa huenda akawa amezaliwa asiku wa kuamkia leo na kutupwa na hadi kupatikana, alikuwa amekwisha kufa kutokana na baridi.

Mwili wa mtoto huyo umegunduliwa na akina mama waliokuwa wakitupa taka katika dampo hilo na kutoa taarifa kwa maafisa Afya pamoja na polisi ambao wamefika eneo la tukio na kuuchuku mwili huo huku juhudi za kumbaini aliyefanya kitendo hicho zikiwa zinaendelea.



Ni wapi dunia hii inaelekea?

Post a Comment

 
Top