Mlinzi wa maduka matatu mjini Njombe Adamu Kiswaga mkazi wa mtaa wa Ramadhani mwenye umri Kati ya miaka 45-50 ameuawa na watu wasiofahamika usiku wa Kuamkia jana akiwa katika eneo lake la kazi

Tukio hilo limetokea majira ya saa nane usiku katika eneo la nyumba ya  kulala wageni ya Amani Lodge mkabala na Kituo Cha Mafuta Cha GAPCO Ambapo Mlinzi Huyo Ameuawa kwa kupigwa na Kitu Kizito Kichwani Wakati Akiwa Lindoni.

Baadhi ya Mashuhuda na Walinzi Waliokuwepo Katika Eneo la Tukio Wamesema  Mlinzi Huyo Ameuawa na Watu Wawili Ambao Hawakuweza Kuwatambua Wakati Wakitaka Kujaribu Kubomoa  duka la Mzee Makete.

Mara
baada ya majambazi kutekeleza mauaji hayo ghafla walijitokeza Walinzi toka Maeneo Mengine na kuanza  kupambana bila ya silaha za moto kisha maharamia hao wakapata mwanya wa kutoroka na kutokomea kusiko julikana.

Baadhi ya Wahudumu na Wateja Waliolala Katika Nyumba Hiyo Wamesema Kuwa Mara Nyingi Walinzi Katika Eneo Hilo Wamekuwa Wakiota Moto Nyuma ya Nyumba Hiyo Katika Jiko la Kuchemshia Maji huku wakiacha malindo yao bila ulinzi.

Kwa mujibu wa maelezo ya mmiliki wa nyumba hiyo Rodgers Mhagama amesema mlinzi huyo alikuwa akilinda Kwa Kutumia silaha za Jadi  hali Iliyosababisha mlinzi kuzidiwa nguvu.


 
 Gari la polisi katika eneo la tukio.                                                                                                                                  
 
Mwili wa marehemu ukiwa ndani ya gari la polisi ukisafirishwa kupelekwa chumba cha kuhifadhia maiti.

Post a Comment

 
Top