Wananchi nchini Nigeria wameandamana na
kuitaka serikali ya Rais Goodluck Jonathan kutoeneza machafuko katika
maeneo ya kaskazini mwa nchi hiyo.
Matamshi hayo yametolewa kwenye
maandamano yaliyofanyika katika mji mkuu Abuja kupinga kutekwa nyara
wanafunzi wasichana wa shule na kundi la kitakfiri la Boko Haram.
Oby Ezekwesili, mratibu wa kampeni ya
‘Warejesheni Wasichana Wetu’ amesema Rais Jonathan anapaswa kuangalia
upya stratejia za serikali katika kukabiliana na ugaidi Nigeria.
Ameongeza kuwa, ni muhimu kwa rais huyo Amiri jeshi mkuu wa jeshi
kujadiliana na timu ya usalama na kuangalia tena stratejia za operesheni
hiyo.
Maandamano hayo yamefanyika wakati siku
ya Alkhamisi watu wenye silaha walishambulia kijiji cha Gurmushi
kaskazini mwa Nigeria na kuua watu wasiopungua 32.
Rais Goodluck
Jonathan alitangaza siku hiyo pia kuwa ameamuru kufanywa operesheni kali
dhidi ya kundi la Boko Haram na kuvitaka vikosi vya usalama kuchukua
kila hatua kuhakikisha kwamba kundi hilo linasambaratishwa.
Tehran.
Post a Comment