Eneo ambako miili ya wasichana waliobakwa ilipatikana ikining'inia kwenye mti.
Watu nchini India wameghadhabishwa na uzembe wa polisi katika jimbo la Uttar Pradesh kufuatia tukio la wasichana wawili kubakwa na kuuawa na mili yao kuwekwa juu ya mti.

Baba mzazi wa mmoja wa wasichana hao amesema kuwa polisi walimkejeli alipokwenda kutaka usaidizi wa kumtafuta msichana wake aliyetoweka kabla ya kupatikana akining'inia kwenye mti na mwenzake.
Alisema kuwa wakati polisi walipogundua kuwa anatoka katika tabaka linalotazamiwa kuwa la hadhi ya chini, walikataa kumsaidia kutafuta msichana wake.

Watu watatu akiwemo polisi mmoja wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo.

Familia za waathiriwa zimelalamika kwamba polisi walikataa kuwasaidia kutafuta wasichana hao waliokuwa na umri wa miaka 14 na 16 mtawalia na ambao pia wanatoka familia moja.

"nilipokwenda kwa polisi, kitu cha kwanza nilipoulizwa ni tabaka langu , nilipowaambia wakaanza kunitukana, '' alisema baba huyo wa mmoja wa wasichana hao waliobakwa kisha kuuawa.
Polisi walisema kuwa wanaume hao walikamatwa kwa kuwabaka kisha kuwaua wasichana hao.

Polisi mmoja pia alizuiliwa kwa kushirikiana na washukiwa na pia kwa kukosa kuchukua hatua. Bado mshukiwa mmoja anasakwa na polisi.

BBC Swahili.

Post a Comment

 
Top