Wasichana wawili wa kihindi wanaokadiriwa kuwa na umri wa miaka kati ya 13/15waliopatikana wakiwa wananing'inia kwenye mti katika jimbo la Uttar Pradesh, wamekutwa wakiwa wamebakwa kisha kuuawa.

Kwa mujibu wa polisi nchini humo mpaka sasa mwanamume mmoja amekamatwa kuhusiana na mauaji hayo na polisi watatu wakiachishwa kazi kwa kutosajili kesi hiyo mara tu baada ya kuripotiwa kuwa wasichana hao walikuwa wametoweka, kabla ya kupatikana wakiwa wameuawa.

.

Visa vya dhuluma za kingono vimeendelea kukithiri nchini India tangu mwaka 2012 ambapo msichana mmoja alibakwa na genge la vijana hadi kufa huku hali ya ubaguzi dhidi ya wanawake ukizidi kuotesha mizizi ndani ya jamii nchini India.

Serikali ililazimika kuweka sheria kali kwa wanaopatikana na hatia ya kutenda vitendo vya dhuluma za kingono baada ya maandamano kufanyika kote nchini kufuatia shambulizi hilo.

Polisi mmoja ambaye alihojiwa na BBC alidai kuwa wasichana hao walikuwa na uhusiano wa kifamilia na walipatwa wakiwa wananing'inia kwenye mti kijiji cha Badaun mnamo siku ya Jumatano.


Wasichana hao walichomwa kutokana na tamaduni za maziko ya kihindi siku ya Jumatano.

Post a Comment

 
Top