Kaimu meneja wa uhamasishaji katika kampeni hiyo   Bertha Dennis ambaye pia ni mtangazaji wa kipindi cha VUTA PUMZI na MORNING EXTRA.
Kwa mara ya kwanza kituo bora cha matangazo kutoka Nyanda za juu kusini, Redio ebony fm imezindua kampeni maalumu ya kuwafikia wananchi katika maeneo ya vijijini kama njia ya kuwaunganisha pamoja watanzania.

Kampeni hiyo inayoitwa
Ni wewe! ambayo imezingduliwa mapema leo chini ya jopo la wafanyakazi wa kituo hicho imelenga kumfikia msikilizaji ambaye hakuwahi kufikiria kufikiwa na redio hiyo ikiwa ni pamoja na kung’amua changamoto za mazingira.

Akizungumza na  Ramani Ulimwengu  jiono hii, Kaimu meneja wa uhamasishaji katika kampeni hiyo   Bertha Dennis amesema kampeni hiyo itakayo ambatana na uhamasishaji wa maonesho ya kilimo ya nane nane, ambapo timu ya wafanya kazi inataraji kuyafikia baadhi ya maeneo ya vijjini.

Miongoni mwa Wajumbe katika kampeni hiyo Raymond Fransis na Nikison Sanga  wamebainisha nia ya kampeni yao na kuwaomba wakazi wa maeneo ya vijijini watakao pata fursa ya kufikiwa na timu hiyo kuwaunga mkono.

Kampeni ya NIWEWE! itakuwa ni kampeni endelevu ambayo itaanza rasmi tarehe 15/July/ 2014 katika kata ya Itunundu wilayani Iringa na baadaye timu ya wahamasishaji itatembelea maeneo ya Vwawa Mbozi mkoani Mbeya na kisha kumalizikia mkoani Njombe.

Post a Comment

 
Top