"Jambo beat" bila shaka jina hili linakukumbusha vitu vingi sana msikilizaji wa Ebony fm radio kutoka nyanda za juu kusini kutokana na umahili wa kipindi hiki cha redio.

Kipindi cha Jambo beat ambacho kinaanza saa 04:00 asubuhi mpaka saa 07:00 mchana na kukupa nafasi msikilizaji kuifurahia siku yako kwa kupata taarifa za ma-supa star kibao wa bongo, skenndo za wanasiasa, mipasho, habari za kipelelezi na burudani za muziki, kwa sasa kipindi hiki kimekuwa midomoni mwa watu kutokana na dhima na staha za watangazaji katika kipindihicho.

Wengi humuita Dereva mtundu, Kibwagala, Kubwa la maadui lakini majina yake kamili ni Aisha Sandiga mtangazaji aliyejizolea umaarufu kutokana na umahiri wake katika fani ya utangazaji, mipangilio ya burudani, sauti aliyojaaliwa na yeye kuitendea haki na kuteka mamilioni ya wasikilizaji kutenga muda wao na kukitegea sikio kipindi hiki.

Katika kipindi cha Jambo beat chenye ujazo wa kutosha na kutokana na umaridadi wa watangazaji wake utapata fursa ya kuwasikia watangazaji viunzi katika segmeti mbalimbali ndani ya Kipindi ikiwa ni pamoja na Ripoti za Mpelelezi ambazo hudondoshwa na mtangazaji mwenye sauti nzito na kumfanya awe wapekee Robinson Msuva (Robby Daby).

Na katika mipasho utasikia Kaogeeeee!  muda ambao wanafiki na mapashkunaz hujikuta katika wakati mgumu kutokana na tabia zao za umbea, hapa utamsikia bi. Tinna Tana akidondosha kauli zake ambazo huwafanya wasikilizaji wasibandue masikio kwenye redio wakati huo.

 Aisha Sandiga katika pozi mara baada ya kumaliza show.
 Robinson Msova (Robbydaby) Mpelelezi, kijana ambaye sauti yake imekuwa ikifananishwa na mtangazaji wa Times fm Gadna habash, ambaye licha ya kusikika katika ripot za mpelelezi ya Jambo beat Kinda huyu utamsikia katika LOVENET kuanzia saa 04:00 usiku mpaka 07:00 usiku wakiwa na Agnes Andason (Manzi wa TZ).
 Mamaa wa mipasho, Tinna Tana ambaye licha ya kusikika katika segment ya Kaogee! ya Jambo beat lakini pia ni mtangazaji wa kipindi cha Raha zote kila siku ya juma mosi.
Mpelelezi

Post a Comment

 
Top