Wananchi wa Itunundu Pawaga wilayani Iringa wakiisubiri timu ya Ebony fm siku ya jumamnne katika ziara ya kwanza ya Ni wewe Kampeni.

 Raimond Francis mtangazaji wa kipindi cha Morning talk akizungumza na wafanyabiashara wa Itunundu
 Miongoni mwa akina mama wajasiriamali wakifanya biashara zao ndogondogo kijijini Itunundu
 Timu ya wafanyakazi wa ebony fm ikitua Itunundu katika ziara ya kwanza ya Ni wewe kampeni.
 Umati wa watu waliojipanga kuilaki timu ya Ebony fm.
 Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari ni miongoni mwa waliojitokeza katika Ni wewe kampeni.
 Raymond francis Challi mtangazaji wa kipindi cha Morning talk akiwasalimu wananchi wa Itunundu.





Ziara ya kwanza ya ufunguzi wa kampenni ya NI WEWE inayofanywa na ebony fm katika mikoa yote ya nyanda za juu kusini ambayo imeanza  kwa kuwatembelea wakazi wa kijiji cha Itunundu katika kata ya Pawaga wilayani Iringa mapema jana , wananchi katika kata hiyo jana wamekuwa ni mashuhuda namba moja wa Kampeni hiyo.

Pamoja na shamra shamra za siku hiyo miongoni mwa wananchi wamejipatia majokofu yasiyo tumia umeme kama walivyo ahidiwa mapema asubuhi ya leo akizungumza na kwa njia ya simu na Ramani ya Ulimwengu ya Ebony fm mwenyekiti wa kijiji cha Itunundu Joseph Malinga amekiri  kuwa ujio huo umetoa hamasa ya mshikamano mongoni mwa wananchi.
 

Timu nzima ya NI WEWE Campaign ya Ebony fm kwa sasa inajipanga kuelekea katika kijiji cha Kipengere kilichopo wilayani Wanging’ombe mkoani Njombe ikiwa na lengo la kutoa shukrani kwa wasikilizaji pamoja na kujifunza jiografia ya mazingira ya wasikilizaji hao.

Mwenyekiti wa kijiji cha kipenge Hawad Mwanganya mbaye pamoja na kuikaribisha ebony fm katika eneo lake lakinia amewata wananchi wa eneo hilo kujitokeza kwa wingi kwa ni kufika kwa timu hiyo ni faraja kwa wakazi huku akikiri kuwa hiyo itakuwa ni mara ya kwanza kwa wananchi wake kutembelewa na redio.

Ni wewe Campaign yenye lengo la kuwaunganisha wakazi wa mikoa ya nyandanda za juu kusini mara tu baada ya kutimua vumbi katika ardhi ya kipengele mapema siku ya tarehe 18 July mwaka huu kivumbi kitahamia mkoani Mbeya ambako wakazi katika wilaya ya Mbozi mkoani humu wataipokea timu hiyo.

Post a Comment

 
Top