Israeli imeendelea kuivirumishia makombora Gaza kucha
kutwa ,huku kikao cha mawaziri wa baraza la Usalama kikitarajiwa huko
Marekani kujadili mapendekezo mapya ya wito wa kusitishwa mapigano kwa
misingi ya kibinadamu.
Idadi ya raia wa Palestina waliouawa imezidi mia nane, huku mashambulio hayo ya Israel ya angani majini na ardhini yakiingia siku ya kumi na nane.
Wanajeshi 32 na raia watatu wa Israel wameuawa katika muda huo.
Katika ukingo wa magharibi, na Jerusalem mashariki raia wawili wa Palestina wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa wakati waandamanaji waliokuwa na hasira kuhusu mashambulio huko Gaza walipokabiliana na vikosi vya Israel.
Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki Moon anasema ameshtushwa na kushambuliwa kwa shule ya Umoja huo iliyopo huko Beit Hanoun, ambako mamia ya watu walifika kutafuta hifadhi.
Hata hivyo Bwana Moon na waziri wa maswala ya kigeni wa Marekani John Kerry wanaendeleza juhudi za kutafuta makubaliano ya kusitisha vita.
Kerry alikuwa Cairo kukutana na waziri wa maswala ya kigeni wa Misri Sameh Shoukry na Ban Ki-moon ambapo wanajaribu kuishinikiza Hamas kukubali mwito wa kusitisha mapigano bila ya kuishinikiza Isareli kuondoa vikosi vyake katika ukanda wa Gaza.
BBC-Swahili.
Post a Comment