Imeelezwa kuwa, huenda Kenya ikakumbwa na uhaba wa chakula hasa katika maeneo ya vijijini na kusini mashariki mwa nchi hiyo.

Utafiti uliofanywa unaonyesha kuwa, kiwango cha mvua kati ya Machi na Mei mwaka huu katika maeneo mengi ya Rift Valley kilikuwa cha chini ikilinganishwa na kiwango chake cha kawaida.

Watabiri wa hali ya hewa wanasema kuwa, kiwango cha mvua kinatarajiwa kupungua pia katika miezi ya Julai mpaka Septemba hali ambayo huenda ikapelekea kupungua mno mavuno kati ya Oktoba hadi Februari mwakani.

Wizara ya Kilimo ya Kenya imetangaza kuwa, kiwango cha mazao kwa mwaka huu bila ya shaka kitakuwa kidogo ikilinganishwa na mwaka jana.

"Kupungua mavuno kunatokana na kupungua uzalishaji katika maeneo mbalimbali ya Rift Valley hali ambayo imetokana na ukame mtawalia katika miezi ya Aprili na Mei," imebainisha taarifa ya Wizara ya Kiliomo ya Kenya.

Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, idadi ya watu wasio na usalama wa kutosha wa chakula nchini Kenya ilifikia milioni moja, laki mbili na tisini elfu mwezi Februari mwaka.
Radio Tehran.

Post a Comment

 
Top