Wavulana 19 wamefariki dunia katika kipindi cha miezi 6 tangu kuunza mwaka 2014 katika sherehe za kitamaduni za tohara kwa wavulana (Jando)nchini Afrika kusini .

Utamaduni wa tohara ni muhimu kwa vijana hasa kwa kuwa ni njia ya vijana kuingia utu uzima, lakini baadhi hufariki wakipitia utamaduni huo na wengine hupoteza sehemu za viungo vyao.

licha ya idadi ya vifo hivyo kuripotiwa, lakini mpaka sasa wapo wengine 50  ambao wako hospitalini wakipokea matibabu kutokana na kukosa maji mwilini na sehemu zao za siri kuoza pamoja na  majerahe mengine.

Wazee wa kijamii wasiokuwa na mafunzo ya kufanya tohara ambao huendesha vituo vya tohara kwa vijana wamelaumiwa kwa vifo kama hivyo.

Katika baadhi ya visa ambavyo vimeripotiwa, vijana hutoroka na kujiunga na vijana wengine wanaokwenda katika vituo hivyo haramu bila ya idhini ya wazazi.

Serikali imewasihi wazee wa kijamii kushirikiana na watu wenye uwezo wa kitaalamu na madaktari ili kuwapasha tohara vijana na kuzuia vifo.

Mwezi jana watu 23 walikamatwa kwa vifo vya vijana waliofariki kutokana na athari za kupashwa toihara
.

BBC-Swahili

Post a Comment

 
Top