Oscar Pistorius
Mwanariadha wa Afrika Kusini asiye na miguu yote
miwili Oscar Pistorius ameathirika vibaya kutokana na ulemavu wake,
daktari wa michezo ameiambia mahakama inayosikiliza kesi ya mauaji
inayomkabili mwanariadha huyo.
Bwana Pistorius anasema alimuua kwa kumpiga risasi rafiki yake wa kike Reeva Steenkamp baada ya kumdhania ni mwizi aliyeingia ndani ya nyumba yao mwaka jana.
Upande wa mashitaka unasema kuwa Pistorius alimuua kwa makusudi Bi Steenkamp baada ya kuzozana.
Suala linaloangaliwa ni akili ya Pistorius wakati akifyatua risasi dhidi ya Reeva.
BBC-Swahili.
Post a Comment