Taasisi zinazofungamana na Umoja wa Mataifa zimeitaka jamii ya kimataifa kuisaidia Somalia ili kuzuia kuibuka mgogoro wa chakula katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu na Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa UNICEF zimetaka Somalia ipatiwe misaada.

 John Ging, mratibu wa operesheni katika Idara ya Kuratibu Misaada ya Kibinaadamu ya Umoja wa Mataifa amesisitiza kwamba, kuna kila dalili za Somalia kukumbwa na uhaba mkubwa wa chakula.

Ameongeza kuwa, ukosefu wa amani, kuongezeka kwa bei za bidhaa za chakula na kupungua mvua ni mambo ambayo yanabainisha udharura wa kuchukuliwa hatua za maana kwa shabaha ya kuzuia kutokea matatizo makubwa ya ukosefu wa chakula nchini Somalia.

Somalia ingali inataabika na ukame mkubwa ulioikumba nchi hiyo mwaka 2011 na kusababisha hasara kubwa hususan eneo kubwa la kusini mwa nchi hiyo ambalo lilikumbwa na ukame na baa la njaa.

BBC-swahili.

Post a Comment

 
Top