Rais wa
Zimbabwe, Robert Mugabe, amewataka wakulima wazungu waliosalia nchini humo kuondokana kuwaachia mashamba wazalendo wa nchi hiyo.
Wakosoaji wa Rais Mugabe, wanasema kuwa sera yake kutaka kumiliki mashamba yote
Mkulima huyu mzungu akitizama uharibifu uliofanywa nyumbani kwake baada ya watu kuivamia
yanayomilikiwa na wazungu, ndio ilisababisha kuzorota kwa uchumi wa nchi hiyo kati ya mwaka
2000-2009.Rais Mugabe mwenye umri wa miaka 90, ametawala Zimbabwe tangu nchi hiyo kujipatia uhuru mwaka 1980 na kuchaguliwa tena mwaka jana kwa asilimia 61 ya kura, na kumshinda mpinzani wake wa jadi Morgan Tsvangirai.
Mdadisi wa kisiasa nchini humo Stanley Kwenda anasema kuwa matamshi ya Mugabe, yanashangaza sana kwani serikali ilimaliza mageuzi ya sera ya umiliki wa mashamba miaka miwili iliyopita.
Inaonekana kwamba Mugabe anataka kuhujumu hali mbaya ya kiuchumi nchini humo kwa kuzungumzia maswala mengine ambayo hayana umuhimu kwa sasa.
Wananchi wa Zimbabwe wanakumbwa na kiwango kikubwa cha ukosefu wa ajira na kufungwa kwa makampuni ambapo mpaka sasa ni wakulima 100 hadi 150 wazungu ndio waliosalia nchini Zimbabwe.
Kwa mujibu wa mkuu wa muungano wa wakulima wazungu nchini Zimbabwe, Hendricks Olivier ni kwamba Matamshi ya Rais Mugabe, yalisababisha wasiwasi miongoni mwa wakulima wazungu nchini humo.
Maelfu ya wakulima walilazimika kuyaacha mashamba yao na kurejea walikotoka baada ya serikali kufanya mageuzi ya sera ya umiliki wa ardhi miaka 15 iliyopita.
Post a Comment