Mtu mmoja amefariki na wengine wengi kujeruhiwa katika shambulizi la bomu jijini Arusha na mpaka sasa
Polisi wamewakamata watu wawili wakihusishwa na
shambulio hilo lililotokea kwenye mgahawa wa 'Vama Traditional Indian
cuisine' jijini humo.Jumla ya Watu 20 wanashikiliwa na Polisi wakiwemo watu sita wanaosadikiwa kujihusisha na mlipuko wa bomu uliotokea mkoani Arusha juma lililopita nyumbani kwa Kiongozi wa dini Sheikh Sudi Ally Sudi na kujeruhi watu wawili.
Polisi wanaendelea na upelelezi kuhakikisha inawatia nguvuni watu waliohusika na matukio hayo.
Haijulikani kilichosababisha mlipuko huo.
Post a Comment