Nani?...au yule...hapana atakuwa huyu....mmm...labda mimi.

Nani atatawazwa kuwa mgombea kiti cha ubunge jimbo la Iringa mjini kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi CCM? maswali kama haya kwa miongoni mwa wapiga kura huenda yakatoa nafasi ya mgombea kupitia chama pinzani kujinyakulia ushindi kwa kishindo.

Lakini sikiliza maneno ya wachumia juani yanaumiza kweli tena yanatoa hamasa kwa watu kuanza kuzitukuza leo zao kwani wapo wasemao kuwa kuendelea kujitokeza kwa makundi ndani ya chama chochote cha siasa ni sehemu ya Demokrasia na ukuaji wa chama husika.

Ila makundi haya ya CCM mbali ya kuwa ni Demokrasia bado ni kete ya ushindi kwa mbunge Msigwa na chama chake kuendelea kuitesa CCM 2015. 

Hadi sasa CCM bado haijawa na mgombea anayejulikana zaidi ya kila mmoja kuendelea kupiga kampeni za chini kwa chini akiutaka ubunge wa jimbo hilo kiasi cha kuwachanganya wapiga kura na hata siku itakapofika ya kura za maoni kwa kuwa kila mwanachama atakuwa amejipitisha na kumwaga sera zake.

Itakuwa ni vigumu kwa makundi kuvunjika hivyo si vibaya kwa vyama vyote vya siasa kujipanga ili kuacha kuchanganya wananchi kwa kipindi hiki ambacho bado muda wa kufanya hivyo kufika.

Nawakumbusha tu watanzania wenzangu kuwa tusiacha mbachao kwa msala upitao, "kwani familia si yangu, hivyo basi hata majukumu nayajua nani atafanya nini kwa wakati gani na kwa minajili ipi" inajibu rangi ya kijani.

Post a Comment

 
Top