Mafurushi ya viungo vya binadamu yalikutwa jalalani hapo
Huku likiendelea na uchunguzi kuhusu tukio hilo,Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova ametangaza kuundwa kwa jopo la upelelezi kuchunguza tukio hilo, ili kubaini taratibu gani zilikiukwa na kujua aina ya mashtaka itakayowakabili.
Uchunguzi wa awali umebainisha kuwa miili hiyo ilikua katika Taasisi ya mafunzo ya udaktari IMTU kabla ya kukutwa imetupwa eneo la Bunju.
Taasisi hiyo imekiri kwamba mabaki ya miili ilikua katika taasisi hiyo lakini haijatoa maelezo kuhusu kutupwa kwa miili hiyo.
Kamanda Kova amewatoa wasiwasi watanzania kuwa hakuna mauaji yoyote ya kimbari yaliyotokea sehemu yeyote nchini hivyo polisi iachiwe ifanye kazi yake kisha itatoa taarifa hapo baadae.
Mapema asubuhi ya leo Taarifa ambazo zimekuwa zikisambazwa na vyombo vya habari lukuki tangu asubuhi ya leo zimekuwa zikihusua viungo mbali mbali vya binadamu ambvyo vimekutwa katika eneo la kutupa taka la Bunju mjini Dar es Salaam katika mazingira ambayo haijafahamika mara moja kuwa viungo hivyo vimetoka wapi.
Mabaki ya mafurushi ya viungo hivyo.
Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova akizunguza na wanahabari.
Post a Comment