Waziri wa habari wa Liberia
Lewis Brown amesema kuwa wagonjwa 17 kati ya 37 waliokuwa katika
zahanati iliyokuwa ikitumika kama kituo cha kuwatenga wagonjwa wa Ebola
hawajulikani waliko.
20 waliosalia wako katika zahanati mbalimbali karibu na mji mkuu Monrovia .
Zahanati moja inaendeshwa na Hospitali kuu ya John F. Kennedy ilihali wengine wako katika zahanati ya ELWA nje ya mji huo.
Wote hao watachunguzwa kabla ya hatua madhubuti kuchukuliwa kwa maslahi ya Umma.
Katika hatua ya kushtua sana wakaazi wa vitongoji vya mji wa Monrovia walivamia zahanati hiyo iliyokuwa ikitumika kama kituo cha kuwatenga wagonjwa wa homa ya Ebola wakaipora na kuwaruhusu wagonjwa kutoroka.
''Kwa sasa tunashughulikia hali hii ilivyo kwani watu sasa wamerejea miongoni mwa jamii na hivyo kueneza maambukizi zaidi''
''Kufuatia uvamizi huo tumejifunza mengi ''
Ajabu ni kuwa watu walikuja ndani ya kituo hicho walijileta huko wenyewe kwa hivyo sisi tunachukulia kuwa labda wagonjwa hao walitaka kusalia huko lakini wakalazimishwa kutoroka kukimbilia maisha yao kwa sababu wavamizi walikuwa wanapora mali ya Westpoint.
Brown alisema kuwa kwa sasa zahanati hiyo ya Westpoint Imefungwa lakini kuna mipango ya kuifungua tena.
''Tunafahamu kuwa kuna watu ambao bado wanashauku iwapo Ebola ipo ama hakuna lakini ukitizama takwimu kutoka jimbo la Lofa utaona kuwa idadi ya wahasiriwa imeanza kupungua.''
Lofa ndiyo iliyokuwa kitovu cha mlipuko ulioko sasa wa homa hii ya Ebola Taharuki ilitanda kote nchini humo ,baada ya kituo kilichotengwa na kuwekewa kwa sababu ya kutoa matibabu kwa wagonjwa wa Ebola, kilishambuliwa na zana kuporwa katika mji mkuu wa Liberia, Monrovia.
Watu 37 waliowekwa hapo kuangaliwa kama wana dalili za Ebola walitoroka baada ya kituo hicho kuporwa Jumamosi usiku.
Washambuliaji walipora magodoro na vitu vingine.
Mwandishi wa BBC katika kanda hiyo anasema pengine washambuliaji walikerwa kuwa kituo hicho kimewekwa katika mtaa wao.
Mafisa wakuu nchini Liberia wanajaribu kuwatafuta wagonjwa waliotoroka ili kuwarejesha tena kwenye kituo hicho.
Watu zaidi ya 400 wamekufa kwa sababu ya ebola nchini Liberia kati ya zaidi ya 1,000 katika kanda ya Afrika Magharibi.
BBC-swahili
Post a Comment