Wa kwanza kushoto ni Makamu mkurugenzi MUVIMA Albert Chalamila, katikati
aliyeshika mpira ndiye Mkurugenzi mkuu MUVIMA Cossato Chumi.
Mashindano ya Kombe la Muvima yaliyomalizika hivi karibuni wilayani Mufindi mkoani Iringa yaligubikwa na sokomoka na kuzua utata baina ya kamati ya uongozi wa mashindano na wadhamini baada ya matokeo kutajwa kuwa batili.
Baada ya mashindano hayo kumalizika mapema mwezi jana, Wadhamini wa mashindano hayo walishikwa na kigugumizi cha kutoa zawadi kwa washindi baada ya timu shiriki kudai kutoridhishwa na mchakato wa upatikanaji wa washindi na kudai kuwa sheria zilikiukwa.
Hali hiyo ilimpelekea mdhamini wa mashindano kurudi na maburungutu ya zawadi kupisha maridhiano baina ya viongozi wa kamati ya mashindano na washiri.
Baada ya mgogoro huo kufikia muafaka, mapema mwishoni mwa wiki iliyopita Mdhamini wa mashindano Mkurugenzi wa asasi ya Muvima Cossato Chumi akiongozana na makamu wake Albert Chalamila ambaye pia na mhadhiri katika chuo kikuu cha Iringa walirejea katika viwanja vya mashindano na kukabidhi jezi pamoja na mipira kwa washindi wa kwanza, wapili na wa tatu.
Wa kwanza kushoto ni Makamu mkurugenzi MUVIMA Albert Chalamila, katikati
aliyeshika mpira ndiye Mkurugenzi mkuu MUVIMA Cossato Chumi.
Umati wa watu waliojitokeza kushuhudia makabidhiano
Wa kwanza kushoto ni Makamu mkurugenzi MUVIMA Albert Chalamila, katikati aliyeshika mpira ndiye Mkurugenzi mkuu MUVIMA Cossato Chumi.
Home
»
»Unlabelled
» MUVIMA YAKABIDHI ZAWANDI KWA WASHINDI LIGI YA KOMBE LA MUVIMA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment