Fulgance Malangalila (kulia), enzi za uhai wake akipokea cheti cha mafunzo ya uandishi wa habari ya muda mfupi. Anayemkabidhi ni Rais wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Kenneth Simbaya.


MWENYEKITI wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Iringa, Frank Leonard anatangaza kifo cha mwanachama wao Fulgance Malangalila (71) aliyefariki usiku wa kuamkia jana baada ya kulazwa kwa takribani wiki moja katika hospitali ya mkoa wa Iringa.
Jitihada za madaktari wa hospitali hiyo kunusuru maisha ya Malangalila aliyekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukuri kwa muda mrefu zilishindikana.
Kabla mauti hayajamkuta, Malangalila alikuwa mwandishi wa kujitegemea akiandika uchambuzi na makala katika vyombo mbalimbali vya habari nchini yakiwemo magazeti ya Business Times na Majira
Ndani ya Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Iringa, Malangalila alikuwa mjumbe wa Kamati Kuu akiongoza kamati ndogo ya maadili (inayosimamia maadili ya waandishi wa habari).
Mzee Malangalila anatarajiwa kuzikwa saa nane mchana wa leo katika makuburi ya Tosamaganga nje kidogo ya Manispaa ya Iringa.

Ibada ya kumuaga itafanyika katika Kanisa Katoliki, Mshindo mjini Iringa saa saba mchana.

Post a Comment

 
Top